Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday 13 October 2017

Kikombe Cha Asubuhi ;Yoshua 4..



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote..
Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu,Muumba wa vyote..
Baba wa upendo,Baba wa Baraka,Baba wa  yatima..
Mungu wa Abrahamu Isaka na Yakobo..
Muweza wa yote,wewe ni mwanzo na wewe ni mwisho..
Utukuzwe Baba wa Mbinguni,Usifiwe Mungu wetu,Uhimidiwe Yahweh,Uabudiwe daima,Unatosha ee Mungu wetu,Hakuna kama wewe ee
Jehovah nissi,Jehovah Jireh,Jehovah Shammah,Jehovah Rapha,Jehova Raah, Emanuel -Mungu pamoja nasi..!!


Asante Baba wa Mbinguni kwa wema na fadhili zako kwetu..
Asante kwa ulinzi wako wakati wote..
Asante kwakutuchagua na kutupa kibali cha kuendelea
kuiona leo hii..
Baba wa Mbinguni si kwamba sisi ni wema sana,wala si kwa nguvu/utashi
wetu sisi kuwa wazima na kuwatayari kuendelea na majukumu yetu..
Mungu wetu ni kwa neema/rehema zako,ni kwa mapenzi yako sisi kuwa hivi tulivyo leo hii..
Sifa na Utukufu tunakurudishia Mungu wetu..

Yesu alisema nao tena kwa kutumia mifano: “Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme aliyemwandalia mwanawe karamu ya harusi. Basi, akawatuma watumishi kuwaita walioalikwa waje harusini, lakini walioalikwa hawakutaka kufika. Akawatuma tena watumishi wengine, akisema, ‘Waambieni wale walioalikwa: Karamu yangu iko tayari sasa; fahali wangu na ndama wanono wamekwisha chinjwa; kila kitu ni tayari; njoni harusini.’ Lakini wao hawakujali, wakaenda zao; mmoja shambani kwake, mwingine kwenye shughuli zake, na wengine wakawakamata wale watumishi wakawatukana, wakawaua. Yule mfalme akakasirika, akawatuma askari wake wakawaangamize wauaji hao na kuuteketeza mji wao. Kisha akawaambia watumishi wake: ‘Karamu ya harusi iko tayari kweli, lakini walioalikwa hawakustahili. Basi, nendeni kwenye barabara na wowote wale mtakaowakuta waiteni waje harusini.’ Wale watumishi wakatoka, wakaenda njiani, wakawaleta watu wote, wabaya na wema. Nyumba ya harusi ikajaa wageni. “Mfalme alipoingia kuwaona wageni, akamwona mtu mmoja ambaye hakuvaa mavazi ya harusi. Mfalme akamwuliza, ‘Rafiki, umeingiaje hapa bila vazi la harusi?’ Lakini yeye akakaa kimya. Hapo mfalme akawaambia watumishi, ‘Mfungeni miguu na mikono mkamtupe nje gizani; huko atalia na kusaga meno.’” Yesu akamaliza kwa kusema, “Wengi wamealikwa, lakini wachache wameteuliwa.”

Yahweh tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na
kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu..
Tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya..
kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya
kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea..
Yahweh tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote..
Jehovah tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu kwa Damu ya mwanao mpedwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti,yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona..

Kisha, Mafarisayo wakaenda zao, wakashauriana jinsi ya kumnasa Yesu kwa maneno yake. Basi, wakawatuma wafuasi wao pamoja na wafuasi wa kikundi cha Herode. Wakamwuliza, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwaminifu, na kwamba wafundisha njia ya Mungu kwa uaminifu; humwogopi mtu yeyote, maana cheo cha mtu si kitu kwako. Haya, tuambie maoni yako. Je, ni halali au la, kulipa kodi kwa Kaisari?” Lakini Yesu alitambua uovu wao, akawaambia, “Enyi wanafiki mbona mnanijaribu? Nionesheni fedha ya kulipia kodi.” Nao wakamtolea sarafu ya fedha. Basi, Yesu akawauliza, “Sura na chapa hii ni ya nani?” Wakamjibu, “Ni ya Kaisari.” Hapo Yesu akawaambia, “Basi, ya Kaisari mpeni Kaisari, na ya Mungu mpeni Mungu.” Waliposikia hivyo wakashangaa; wakamwacha, wakaenda zao.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Biashara,Masomo na vyote tunavyoenda kufanya/kutenda...
Baba wa Mbinguni tukatende kama inavyokupendeza wewe
Mungu wetu ukavitakase na kuvibariki vyote tunavyoenda kutumia/kugusa ukavifunike kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo...
Jehovah tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo..
Mungu wetu nasi tunaomba utupe neema ya kuweza
 kuwabariki wenye kuhitaji..
Mungu wetu tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Yahweh ukatupe sawasawa na mapenzi yako..


Siku hiyo, baadhi ya Masadukayo wasemao wafu hawafufuki walimwendea Yesu. Basi, wakamwambia, “Mwalimu, Mose alisema mtu aliyeoa akifa bila kuacha watoto, lazima ndugu yake amwoe huyo mama mjane, ili ampatie ndugu yake watoto. Basi, hapa petu palikuwa na ndugu saba. Wa kwanza alioa kisha akafa bila kujaliwa watoto, akamwachia ndugu yake huyo mke wake mjane. Ikawa vivyo hivyo kwa ndugu wa pili, na wa tatu, mpaka wa saba. Baada ya ndugu hao wote kufa, akafa pia yule mama. Je, siku wafu watakapofufuka mama huyo atakuwa mke wa nani miongoni mwa wale ndugu saba? Maana wote saba walikuwa wamemwoa.” Yesu akawajibu, “Nyinyi mmekosea kwa sababu hamjui Maandiko Matakatifu wala nguvu ya Mungu. Maana wafu watakapofufuka hawataoa wala kuolewa; watakuwa kama malaika mbinguni. Lakini kuhusu kufufuka kwa wafu, je, hamjasoma yale aliyowaambieni Mungu? Aliwaambia, ‘Mimi ni Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo!’ Basi, yeye si Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa walio hai.” Ule umati wa watu uliposikia hivyo ukayastaajabia mafundisho yake.
Mfalme wa Amani tunaomba amani yako,Upendo,Furaha
vikatawale katika Nyumba/ndoa zetu,watoto,wazazi wetu familia/ndugu na wote wanaotuzunguka,Baba ukatubariki na ukatupe hekima,busara,utu wema, huruma na kuchukuliana...
Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu na ukatupe neema ya kusimamia Neno lako Amri na Sheria zako siku zote za maisha yetu....
Yahweh ukatufanye chombo chema nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..

Mafarisayo waliposikia kwamba Yesu alikuwa amewanyamazisha Masadukayo, wakakutana pamoja. Mmoja wao, mwanasheria, akamwuliza Yesu kwa kumjaribu, “Mwalimu, ni amri ipi iliyo kuu katika sheria?” Yesu akamjibu, “ ‘Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote na kwa akili yako yote’. Hii ndiyo amri kuu na ya kwanza. Ya pili inafanana na hiyo: ‘Mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe’. Sheria yote ya Mose na mafundisho ya manabii vinategemea amri hizi mbili.”
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawaguse kwa mkono wako
wenye nguvu wote wanaotaabika na kuelemewa na mizigo,wagonjwa,wenye shida/tabu,wenye njaa, waliokatika majaribu/mapito,waliokatika vifungo vya yule mwovu na wote walikata tamaa..
Mungu wetu ukawaponye na kuwaweka huru,ukawape neema ya kujiombea na kufuata njia zako,
Baba ukawasamehe wale waliokwenda kinyume nawe Mungu wetu ukawakomboe na kuwasimamisha tena
wote walioanguka,Baba wa mbinguni ukaonekane katika mapito yao, Mungu wetu ukapokee sala/maombi yao wote wakuombao na wakutafutao kwa Imani ukawaongoze na ukawape Amani na  Nuru ikaangaze  katika maisha yao..

Mafarisayo walipokusanyika pamoja, Yesu aliwauliza, “Nyinyi mwaonaje juu ya Kristo? Je, ni mwana wa nani?” Wakamjibu, “Wa Daudi.” Yesu akawaambia, “Basi, inawezekanaje kwamba kwa nguvu ya Roho Mtakatifu Daudi anamwita yeye Bwana? Maana alisema: ‘Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti upande wangu wa kulia, mpaka niwaweke maadui zako chini ya miguu yako.’ Basi, ikiwa Daudi anamwita Kristo ‘Bwana,’ anawezaje kuwa mwanawe?” Hakuna mtu yeyote aliyeweza kumjibu neno. Na tangu siku hiyo hakuna aliyethubutu tena kumwuliza swali.
Mungu wetu tunayaweka haya yote mikononi mwako
tukishukuru na kuamini Mungu wetu u pamoja nasi
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!!

Wapendwa/waungwana asanteni sana kwakunisoma/kuwa nami
Mungu mwenye upendo na baraka aendelee kuwabariki katika yote yampendezayo,msipungukiwe katika mahitaji yenu,Baba akawape sawasawa na mapenzi yake..
Nawapenda.

Mawe ya ukumbusho kumi na mawili

1Taifa zima lilipokwisha vuka mto Yordani, Mwenyezi-Mungu akamwambia Yoshua, 2“Chagua watu kumi na wawili miongoni mwa hao Waisraeli, yaani mtu mmoja kutoka kila kabila, 3uwaagize hivi, ‘Chukueni mawe kumi na mawili kutoka hapa katikati ya mto Yordani, kutoka hapa ilipo miguu ya makuhani, muyachukue mawe hayo, mkayaweke mahali pale ambapo mtalala leo hii.’”
4Yoshua akawaita hao watu kumi na wawili ambao alikuwa amewateua miongoni mwa Waisraeli, kila kabila mtu mmoja, 5akawaambia, “Litangulieni sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mpaka katikati ya mto Yordani. Kila mmoja wenu achukue jiwe begani mwake, jiwe moja kwa ajili ya kila kabila la Israeli. 6Jambo hilo litakuwa ishara kati yenu; na watoto wenu watakapowauliza siku zijazo ‘Je, mawe haya yana maana gani kwenu?’ 7Nyinyi mtawaambia, ‘Sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu lilipopitishwa mtoni Yordani, maji ya mto huo yalizuiliwa yasitiririke!’ Kwa hiyo mawe haya yatakuwa ukumbusho kwa Waisraeli milele.”
8Wale wanaume wakafanya kama walivyoamriwa na Yoshua, wakachukua mawe kumi na mawili kutoka katikati ya mto Yordani, jiwe moja kwa ajili ya kila kabila la Israeli, kama Mwenyezi-Mungu alivyomwambia Yoshua, wakaenda nayo hadi mahali pale walipolala, wakayaweka huko. 9Yoshua akasimika pia mawe kumi na mawili katikati ya mto Yordani, mahali pale ambapo nyayo za makuhani waliobeba lile sanduku la agano zilisimama. Mawe hayo yako huko mpaka hivi leo.
10Wale makuhani waliobeba sanduku la agano, walisimama katikati ya mto Yordani mpaka watu walipomaliza kutekeleza kila kitu ambacho Mwenyezi-Mungu alimwamuru Yoshua awaambie watu; Yoshua alifanya yote ambayo Mose alikuwa amemwamuru. Watu wakaharakisha kuvuka mto, 11na watu wote walipokwisha vuka, wale makuhani wakawatangulia na lile sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu. 12Wanaume wa kabila la Reubeni na la Gadi na nusu ya kabila la Manase waliwatangulia Waisraeli wakiwa na silaha zao, kama vile walivyoagizwa na Mose. 13Watu wapatao 40,000 wakiwa na silaha tayari kwa vita walipita mbele ya Mwenyezi-Mungu wakielekea bonde la mji wa Yeriko. 14Katika siku hiyo Mwenyezi-Mungu akamtukuza Yoshua mbele ya Waisraeli wote, nao wakamheshimu Yoshua maisha yake yote kama walivyomheshimu Mose maishani mwake.
15Kisha Mwenyezi-Mungu alimwambia Yoshua, 16“Waamuru makuhani wanaobeba sanduku la maamuzi, watoke mtoni Yordani.” 17Basi, Yoshua akawaamuru wale makuhani, “Tokeni mtoni Yordani.” 18Hao makuhani waliokuwa wamebeba lile sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu walipotoka katikati ya mto Yordani, na kukanyaga ukingo wa mto, maji ya mto Yordani yakaanza kutiririka tena, na kufurika kama kwanza. 19Waisraeli walivuka mto Yordani katika siku ya kumi ya mwezi wa kwanza, wakapiga kambi huko mjini Gilgali, mashariki ya Yeriko. 20Yoshua akayasimika yale mawe kumi na mawili ambayo waliyachukua kutoka mtoni Yordani, huko Gilgali. 21Kisha Yoshua akawaambia Waisraeli, “Watoto wenu watakapowaulizeni siku zijazo, ‘Je, mawe haya yana maana gani?’ 22Mtawaambia hivi: ‘Taifa la Israeli lilivuka mto huu wa Yordani mahali pakavu.’ 23Mtawaambia kuwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, aliyakausha maji ya mto Yordani kwa ajili yenu mpaka mkavuka, kama alivyokausha bahari ya Shamu, kwa ajili yetu tukavuka, 24ili watu wote wa dunia wajue kuwa mkono wa Mwenyezi-Mungu una nguvu; nanyi mpate kumcha Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, milele.”


Yoshua 4;1-24

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Thursday 12 October 2017

Jikoni Leo;Kahawa(Coffee)...

Habari zenu Waungwana..
Nimatumaini yangu wote hamjambo..
Siku nyingi kidogo nimepotea kwa mambo ya jikoni..
Ni muingiliano wa majukumu tuu..

Haya "Jikoni Leo" ni  Kahawa [Coffee]..
Jee wewe unapenda Kahawa? unaipikaje?unapenda kunywa kahawa wapi?
Kijiweni?kwenye migahawa au Nyumbani?
Hapo ulipo/unapoishi watu wanapenda kunywa Kahawa?
 kahawa inanywewa sana wapi
mkoa/mji gani Tanzania?kwa nini? hali ya hewa inaruhusu?Mazoea?Tamaduni? au....
Nilipokulia mimi Dar es salaam Kahawa ilikuwa kuwa inanywewa sana ..
zamani kidogo kulikuwa na vijiwe vya wazee/wanaume wanacheza karata/bao huku wakijinywea Kahawa
pia kulikuwa  na wauza Kahawa, Kashata wa kupitisha mitaani..
Sina uhakika kama utamaduni huu wa kukaa vijiweni
 kunywa Kahawa na kuongea mawili matatu kama bado upo
hata kama upo lakini umepungua sana..
Unafikiri ni kwa nini?Maendeleo?Sehemu za wazi zimepungua?ubinafsi,Hali ngumu au Vijiwe vipo vya kisasa zaidi(Migahawa]
mikubwa ya ndani imeua Vijiwe/vibaraza vya Kahawa?

Mimi hapa nilipo Kahawa inanyweka sana hasa kipindi hiki kinachokuja cha Baridi ndiyo zaidi...
Hata mimi napenda kunywa Kahawa Nyumbani huwa nakunywa hii kutoka Tanzania ,nikiwa Mtaani ni mpenzi wa Cupccino..

Karibu sana Tunywe Kahawa huku tukipeana story/kubadilishana hadithi za maisha,malezi na mengineyo..







"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.



Kikombe Cha Asubuhi ;Yoshua 3..




Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Haleluyah..! mungu wetu yu mwema sana..
Tumshukuru Mungu wetu katika yote..
Asante Baba wa Mbinguni,Mungu wetu,Muumba wetu..
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..
Mfalme wa Amani,Muweza wa yote,Mungu mwenye huruma ,Mungu mwenye kusamehe,Baba wa Upendo,Baba wa Baraka..
Baba wa Yatima,Mume wa wajane,Matendo yako ni makuu mno..
Hakuna kama wewe,Hakuna wa kufanana nawe..
Unastahili sifa,Unastahili kusifiwa,Unastahili kuabudiwa..
Unastahili kuhimidiwa,Unastahili Mungu wetu..


Mfalme wa wa amani tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,
tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako...
Baba wa Mbinguni tunaomba utusamehe dhambi zetu zote
 tulizozifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Mungu wetu nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe
wale wote waliotukosea..
Jehovah tunaomba utuepushe katika majaribu na utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote...
Nguvu za giza,nguvu za mizimu,nguvu za mapepo,nguvu za mpinga Kristo zishindwe katika jina lililo kuu
kupita majina yote jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo..

Yahweh tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu Baba tunaomba
utufunike kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo..

Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Biashara,Masomo na vyote tunavyoenda kufanya/kutenda
Mungu wetu tukatende sawasawa na mapenzi yako..
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo,Mungu wetu nasi tunaomba utupe neema ya
kuweza kuwabariki wenye kuhitaji..
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba ukatupe kama inavyokupendeza wewe..

Mfalme wa amani tunaomba amani ikatawale katika nyumba/ndoa
zetu,watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Mungu wetu tunaomba ulinzi wako,Baraka,Baba wa Mbinguni
ukatamalaki na kutuatamia,ukatuongoze katika kunena na kutenda
Baba tukanene/kutenda yanatokupendeza wewe..
Mungu wetu ukatupe neema ya kusimamia Neno lako Amri na
Sheria zako siku zote za maisha yetu..
Tukawe barua njema nasi tukasomeke kama inavyokupendeza wewe..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na
 tukawe na kiasi...


Mwenyezi-Mungu asema: “Piga kelele, wala usijizuie; paza sauti yako kama tarumbeta. Watangazie watu wangu makosa yao, waambie wazawa wa Yakobo dhambi zao. Siku hata siku wananijia kuniabudu, wanatamani kujua mwongozo wangu, kana kwamba wao ni taifa litendalo haki, taifa lisilosahau sheria za Mungu wao. Wananitaka niamue kwa haki, na kutamani kukaa karibu na Mungu. “Nyinyi mnaniuliza: ‘Mbona tunafunga lakini wewe huoni? Mbona tunajinyenyekesha, lakini wewe hujali?’ “Ukweli ni kwamba wakati mnapofunga, mnatafuta tu furaha yenu wenyewe, na kuwakandamiza wafanyakazi wenu! Mnafunga, na kugombana na kupigana ngumi. Mkifunga namna hiyo maombi yenu hayatafika kwangu juu. Mfungapo, nyinyi mnajitaabisha; mnaviinamisha vichwa vyenu kama unyasi, na kulalia nguo za magunia na majivu. Je, huo ndio mnaouita mfungo? Je, hiyo ni siku inayokubaliwa nami? “La! Mfungo ninaotaka mimi ni huu: Kuwafungulia waliofungwa bila haki, kuziondoa kamba za utumwa, kuwaachia huru wanaokandamizwa, na kuvunjilia mbali udhalimu wote! Mfungo wa kweli ni kuwagawia wenye njaa chakula chako, kuwakaribisha nyumbani kwako maskini wasio na makao, kuwavalisha wasio na nguo, bila kusahau kuwasaidia jamaa zenu. “Mkifanya hivyo mtangara kama pambazuko, mkiwa wagonjwa mtapona haraka. Matendo yenu mema yatawatangulia, nami nitawalindeni kutoka nyuma kwa utukufu wangu. Ndipo mtakapoomba, nami Mwenyezi-Mungu nitawaitikia; mtalia kwa sauti kuomba msaada, nami nitajibu, ‘Niko hapa!’ “Kama mkiiondoa dhuluma kati yenu, mkiacha kudharau wengine na kusema maovu, mkiwapa chakula kwa ukarimu wenye njaa, mkitosheleza mahitaji ya wenye dhiki, mwanga utawaangazia nyakati za giza, giza lenu litakuwa kama mchana. Mimi Mwenyezi-Mungu nitawaongozeni daima, nitatosheleza mahitaji yenu wakati wa shida. Nitawaimarisha mwilini, nanyi mtakuwa kama bustani iliyomwagiliwa maji, kama chemchemi ya maji ambayo maji yake hayakauki kamwe. Magofu yenu ya kale yatajengwa; mtajenga upya juu ya misingi iliyoachwa zamani. Nanyi mtaitwa watu waliotengeneza upya kuta, watu waliozifanya barabara za mji zipitike tena.
Yahweh tazama wenye shida/tamu,wagonjwa,wenye njaa/dhiki
walio dhulumiwa,waliokata tamaa,waliokatawaliwa,
wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali,walio katika
vifungo vya yule mwovu na wote wataabikao na kuelemewa
na mizigo,Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako
wenye nguvu,Baba ukawape uponyaji wa mwili na roho..
Yahweh tunaomba ukawafungue na ukawape neema ya kuweza
kujiombea,Mungu wetu ukawasamehe wale waliokwenda kinyume nawe
Baba wa Mbinguni tunaomba usikie kulia kwao na ukawafute machozi yao,Jehovah tazama wanaokumba na kuamini Baba ukasikie kuomba kwao ukapokee maombi/sala zao..
Baba ukaonekane katika mapito yao na ukawabariki..
Neema zako,Baraka zako,Huruna yako na uponyaji wako vikawafuate watoto wako...

“Kama ukiacha kufanya kazi siku ya Sabato, ukaacha shughuli zako siku yangu hiyo takatifu; kama ukiifanya siku yangu kuwa ya furaha, ukaiheshimu siku hiyo takatifu ya Mwenyezi-Mungu, ukaacha na shughuli zako na kupiga domo, utapata furaha yako kwangu mimi Mwenyezi-Mungu, nitakupatia ushindi katika kila pingamizi nchini, nitakulisha mali ya Yakobo, babu yako. Mimi, Mwenyezi-Mungu, nimesema.”

Asante Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi
mwako tukiamini Mungu wetu u pamoja nasi..
Sifa na Utukufu tunakurudishia ee Mungu wetu..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina...!!
Asanteni sana wapendwa/waungwana kwakuwa nami
Baba wa neema/rehema aendelee kuwaneemesha katika
yote yampendezayo,Baraka na amani ziwafuate..
Nawapenda.


Waisraeli wanavuka mto Yordani
1Asubuhi na mapema Yoshua pamoja na watu wote wa Israeli walianza safari kutoka Shitimu. Walipoufikia mto Yordani, walipiga kambi hapo kwa muda kabla ya kuvuka. 2Baada ya siku tatu, viongozi walipita katikati ya kambi hiyo, 3wakawaambia watu, “Mtakapoliona sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, limebebwa na makuhani Walawi, mtaondoka na kulifuata; 4ndivyo mtakavyojua njia ya kupita maana hamjapita huku kamwe. Lakini msilikaribie mno sanduku la agano; muwe umbali wa kilomita moja hivi.”
5Yoshua akawaambia watu, “Jitakaseni kwa kuwa kesho Mwenyezi-Mungu atatenda maajabu kati yenu.” 6Kisha akawaambia makuhani, “Chukueni sanduku la agano, mtangulie nalo mbele ya watu.” Nao wakalichukua na kutangulia mbele ya watu.
7Mwenyezi-Mungu akamwambia Yoshua: “Leo hii, nitaanza kukutukuza mbele ya watu wote wa Israeli ili wajue kwamba, kama vile nilivyokuwa pamoja na Mose, ndivyo pia nitakavyokuwa pamoja nawe. 8Utawaamuru hao makuhani wanaobeba sanduku la agano wasimame karibu na ukingo wa mto Yordani wakati watakapofika huko.”
9Kisha Yoshua akawaambia Waisraeli: “Njoni karibu mpate kusikia maneno ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.” 10Yoshua akaendelea kusema, “Sasa mtajulishwa kabisa kwamba Mungu aliye hai yu miongoni mwenu na kwamba atawafukuza mbele yenu Wakanaani, Wahiti, Wahivi, Waperizi, Wagirgashi, Waamori na Wayebusi, bila kushindwa. 11Tazameni, sanduku la agano la Bwana wa dunia yote, liko karibu kupita mbele yenu kuelekea mtoni Yordani. 12Sasa, chagueni watu kumi na wawili kutoka makabila ya Israeli, kila kabila mtu mmoja. 13Wakati nyayo za makuhani wanaobeba sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu, Bwana wa dunia yote, zitakapoingia katika maji ya mto Yordani, maji ya mto huo yataacha kutiririka. Na yale yatakayokuwa yanatiririka kutoka upande wa juu yatajikusanya pamoja kama rundo.”
14Basi, watu waliondoka katika kambi zao ili kwenda kuvuka mto Yordani, nao makuhani wakiwa wamebeba sanduku la agano wanawatangulia watu. 15Na mara tu hao waliobeba sanduku la agano walipofika Yordani na nyayo zao zilipokanyaga ukingoni mwa mto huo (mto Yordani hufurika wakati wa mavuno), 16maji yaliyokuwa yanatiririka kutoka upande wa juu yalisimama na kurundikana mpaka huko Adamu kijiji kilicho karibu na mji wa Sarethani. Maji yaliyokuwa yanateremka kwenda bahari ya Araba, yaani Bahari ya Chumvi, yalitoweka kabisa, watu wakavuka mbele ya Yeriko. 17Wakati Waisraeli walipokuwa wanavuka makuhani waliokuwa wanalibeba sanduku la agano walisimama mahali pakavu katikati ya mto Yordani mpaka taifa lote likavuka.


Yoshua 3;1-17

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Wednesday 11 October 2017

Kikombe Cha Asubuhi ;Yoshua 2..





Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote..

Mtakatifu..!Mtakatifu..!Mtakatifu..! Mungu wetu..
Muumba wetu,Muumba wa Mbingu, Nchi na vyote vilivyomo..
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..
Mlinzi wetu,Kimbilio letu,Muweza wa yote,
Hakuna jambo lolote lilogumu kwako Mungu wetu,Unatosha Yahweh..

Neno la Mwenyezi-Mungu lililomjia Yeremia mnamo mwaka wa kumi wa utawala wa Sedekia, mfalme wa Yuda, ambao ulikuwa mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Nebukadneza. Wakati huo, majeshi ya mfalme wa Babuloni yalikuwa yakiuzingira mji wa Yerusalemu, naye nabii Yeremia alikuwa amezuiliwa katika ukumbi wa walinzi uliokuwa ndani ya ikulu ya mfalme wa Yuda. Maana Sedekia, mfalme wa Yuda, alikuwa amemfunga Yeremia akisema, “Kwa nini unatabiri na kusema: ‘Mwenyezi-Mungu asema hivi: Tazama, mimi nautia mji huu mikononi mwa mfalme wa Babuloni, naye atauteka. Sedekia, mfalme wa Yuda, hataepa kutiwa mikononi mwa Wakaldayo; hakika atatekwa na mfalme wa Babuloni, ataonana naye uso kwa uso na kuongea naye ana kwa ana. Sedekia atachukuliwa hadi Babuloni, naye atakaa huko mpaka nitakapomchukulia hatua. Hata kama Sedekia atapigana na Wakaldayo, hatashinda.’” Yeremia akasema, Mwenyezi-Mungu alinena nami akasema: “Hanameli, mwana wa baba yako mdogo Shalumu, atakujia na kusema: ‘Nunua shamba langu lililoko Anathothi, maana wewe ni ndugu yangu kabisa, na unayo haki ya kulikomboa.’” Kisha binamu yangu Hanameli alinijia katika ukumbi wa walinzi kama alivyonifahamisha Mwenyezi-Mungu, akaniambia, “Nunua shamba langu lililoko Anathothi katika nchi ya Benyamini maana wewe una haki ya kulikomboa. Linunue kwa faida yako.” Ndipo nilipotambua kwamba lilikuwa kweli neno la Mwenyezi-Mungu. Basi, nililinunua shamba hilo lililoko Anathothi, kutoka kwa binamu yangu Hanameli, nikamlipa bei yake shekeli kumi na saba za fedha. Nikaitia sahihi hati ya kumiliki, nikaipiga mhuri, nikawaita mashahidi na kuipima ile fedha katika mizani. Kisha, nilichukua ile hati ya kumiliki niliyoipiga mhuri, ambayo ilikuwa na masharti na kanuni, pamoja na nakala nyingine iliyokuwa wazi. Nilimpa hiyo hati ya ununuzi Baruku mwana wa Neria mwana wa Maaseya, mbele ya binamu yangu Hanameli na mashahidi waliokuwa wametia sahihi hati ya ununuzi, na mbele ya Wayahudi wote waliokuwa wameketi katika ukumbi wa walinzi. Mbele ya watu wote hao, nilimpa Baruku maagizo yafuatayo: Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: “Chukua hati hizi zote mbili, hati hii ya kumiliki shamba iliyotiwa sahihi, na hii nyingine iliyo wazi, uziweke katika chungu ili zipate kuhifadhiwa kwa muda mrefu.” Maana Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: “Nyumba na mashamba, pamoja na mashamba ya mizabibu katika nchi hii yatanunuliwa tena.” Baada ya kumkabidhi Baruku mwana wa Neria, hati ya kumiliki shamba nilimwomba Mwenyezi-Mungu nikisema:
Unastahili kuabudiwa,Unasthahili kusifiwa,Unastahili kuhimidiwa
Hakuna kama wewe Mungu wetu..Alfa na Omega..!
Baba wa mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,
tukijishusha,tukijiachilia mikononi mwako ..
Yahweh tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya..
Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Jehovah nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe
wale wote waliotukosea..
Mungu wetu tunaomba utuepushe katika majaribu Baba utuokoe
na yule mwovu na kazi zake zote..
Yahweh tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni utufunike kwa Damu ya Bwana wetu
Yesu Kristo wa Nazareti,yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona..

Ee Mwenyezi-Mungu, ni wewe ambaye kwa nguvu zako nyingi na uwezo wako mkuu, umeziumba mbingu na dunia; hakuna kisichowezekana kwako. Wewe unaonesha fadhili zako kwa maelfu ya watu; lakini pia unawaadhibu watu kwa sababu ya dhambi za wazee wao. Wewe ni Mungu mkuu, mwenye nguvu, Mwenyezi-Mungu wa Majeshi ndilo jina lako. Wewe unapanga kwa hekima na unafanya maajabu; njia za watu wote ziko wazi mbele yako, unamlipa kila mmoja kadiri ya njia zake na matendo yake. Katika nchi ya Misri ulifanya maajabu, ukatenda miujiza, na unaendelea kufanya hivyo mpaka leo miongoni mwa Waisraeli na katika mataifa mengine pia, jambo ambalo limekufanya ujulikane kila mahali. Kwa maajabu na miujiza uliyowatisha nayo Wamisri, uliwatoa watu wako Misri kwa nguvu zako nyingi na uwezo wako mkuu. Uliwapa nchi hii ambayo uliahidi kuwapa wazee wao, nchi inayotiririka maziwa na asali. Nao walifika, wakaitwa na kuimiliki. Lakini wao hawakukusikiliza, wala hawakufuata sheria zako. Hawakutenda mambo uliyoamuru. Ndiyo maana utawafanya wapatwe na balaa hii. Tazama, Wakaldayo wamechimba mahandaki kuuzunguka mji; wameuzingira ili wapate kuuteka; wanaushambulia. Vita, njaa na maradhi vitaufanya mji utekwe na watu hao. Kweli mambo uliyotabiri yametokea. Unaona mwenyewe. Lakini, ee Mwenyezi-Mungu, wewe ndiwe uliyeniambia: “Nunua shamba kwa fedha na kuweka mashahidi,” ingawa mji wenyewe umetekwa na Wakaldayo. Ndipo Mwenyezi-Mungu akaniambia, “Tazama, mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa watu wote. Hakuna lolote linaloweza kunishinda. Kwa hiyo, mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Ninautoa mji huu kwa Wakaldayo na kwa Nebukadneza mfalme wa Babuloni, naye atauteka. Wakaldayo wanaoushambulia mji huu wataingia na kuuchoma moto; watauteketeza pamoja na nyumba ambazo juu ya paa zake ubani ulifukiziwa mungu Baali na tambiko za divai zilimiminiwa miungu mingine, ili kunichokoza. Maana Waisraeli na watu wa Yuda hawakufanya chochote mbele yangu isipokuwa uovu tangu ujana wao; watu wa Israeli hawakufanya chochote isipokuwa kunikasirisha kwa matendo yao. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Mji huu umechochea hasira yangu na kuniudhi tangu siku ulipojengwa mpaka leo hii. Kwa hiyo, nitautoa kabisa mbele yangu, kwa sababu ya uovu wote waliotenda watu wa Israeli na watu wa Yuda, pamoja na wafalme na viongozi wao, makuhani na manabii wao, na wakazi wa Yerusalemu. Wao walinipa kisogo badala ya kunigeuzia nyuso zao; ingawa nimewafundisha tena na tena, wao hawakusikiliza na kuyapokea mafundisho yangu. Waliweka sanamu za miungu yao ya kuchukiza katika nyumba hii inayojulikana kwa jina langu, wakaitia unajisi. Walimjengea mungu Baali madhabahu katika bonde la Mwana wa Hinomu, ili wamtolee mungu Moleki wavulana wao na binti zao, ingawa sikuwaamuru wala sikufikiria kwamba wangefanya hivyo, wakawafanya watu wa Yuda watende dhambi.”

Jehovah tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu,Biashara,masomo
na vyote tunavyoenda kufanya/kutenda Mungu wetu tukatende kama inavyokupendeza wewe..

Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Yahweh nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji..
Mungu wetu tunaomba tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Baba ukatupe sawasawa na mapenzi yako..


Mfalme wa Amani tunaomba amani yako itawale katika
Nyumba/ndoa zetu,watoto,wazazi wetu,famila/ndugu
na wote wanaotuzunguka..

Mungu wetu tunaomba ulinzi wako,
Baba wa Mbinguni tunaomba utamalaki na kutuatamia..
Yahweh tunaomba Baraka zako,Upendo wetu ukadumu,
Hekima,Busara na tuchukulianae..

Yahweh tunaomba utupe neema ya kusimamia Neno lako,Amri na sheria zako siku zote za maisha yetu..

Baba wa Mbinguni utuepushe katika makwazo,migogoro,
kuumizana,chuki,tamaa,unafiki,dhuluma,hasira,kisasi, na yote yanayokwenda kinyume nawe/yasiyokupendeza Mungu wetu..
Ukatufanye chombo chema nasi tukatumike sawasawa na mapenzi yako..

Roho mtakatifu atuongoze katika yote  tukapate kutambua/kujitambua
tukanene yaliyo yako na tukawe na kiasi..


Sasa basi, Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, asema hivi: “Yeremia, watu hawa wanasema kwamba, kwa vita, njaa na maradhi, mji huu utatiwa mikononi mwa mfalme wa Babuloni. Lakini nasema: Nitawakusanya watu kutoka nchi zote ambako kwa hasira na ghadhabu na chuki yangu kubwa, niliwatawanya. Nitawarudisha tena mahali hapa, na kuwafanya wakae salama. Nao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao. Nitawapa moyo mmoja na nia moja, wapate kunicha mimi daima, kwa faida yao wenyewe na kwa faida ya watoto wao watakaofuata. Nitafanya nao agano la milele, kwamba sitaacha kamwe kuwatendea mema; nitaweka mioyoni mwao uchaji wangu ili wasiniache tena. Nitafurahi kuwatendea mema; nitawasimika daima katika nchi hii na kuwatendea kwa uaminifu. “Kama nilivyowaletea maafa watu hawa, ndivyo nitakavyowaletea mema niliyowaahidi. Mashamba yatanunuliwa katika nchi hii ambayo unasema imekuwa ukiwa bila watu wala wanyama, na kwamba imetolewa kwa Wakaldayo. Watu watanunua mashamba kwa fedha, watazitilia sahihi hati zake za kuyamiliki, watazipiga mhuri, na kuweka mashahidi katika nchi ya Benyamini, kandokando ya Yerusalemu, katika miji ya Yuda, katika miji ya nchi ya milima, katika miji ya Shefela, na katika miji ya jangwa la Negebu. Maana nitawastawisha tena. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Mungu wetu tunawaweka mikononi mwako wote wenyew shida/tabu
wagonjwa,wenye njaa,waliokataliwa,waliokata tamaa,
wanaopitia magumu/majaribu,walio katika vifungo vya yule
mwovu na wote walio asi/kuanguka..
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu,Baba ukawape uponyaji wa mwili na roho pia..
Yahweh ukawafungue na wakapate kuwa huru..
Mungu wetu ukawatendee  na ukaonekane katika shida zao..
Baba wa Mbinguni ukawape neema ya kuweza kujiombea
Yahweh ukasikie kulia kwao Baba ukawafute machozi yao..
Jehovah ukapokee sala/maombi yao wote wakuombao kwa moyo na imani..
Mungu wetu ukawasamehe wale wote waliokwenda kinyume nawe Baba ukawanyanyue walioanguka na ukawafariji wafiwa..


Sifa na Utukufu tunakurudishia wewe..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina...!!
Asanteni sana wapendwa/waungwana kwakuwa nami
Mungu Baba aendele kuwabariki na kuwatendea
sawasawa na mapenzi yake..

Amani na Upendo vikadumu ndani yenu
Nawapenda.


Yoshua anawatuma wapelelezi Yeriko

1 Taz Ebr 11:31; Yak 2:25 Basi, Yoshua, mwana wa Nuni, akawatuma watu wawili kwa siri kutoka Shitimu waende kufanya upelelezi, katika nchi ile na hasa mji wa Yeriko. Wakaenda, wakafika kwenye nyumba ya malaya mmoja aliyeitwa Rahabu wakalala humo.
2Mfalme wa mji wa Yeriko akaambiwa, “Tazama, wanaume wawili Waisraeli wameingia mjini leo usiku ili kuipeleleza nchi.” 3Mfalme wa Yeriko akatuma watu kwa Rahabu, akisema: “Watoe nje watu waliokuja nyumbani kwako kwani wamekuja kuipeleleza nchi yote.” 4Lakini, yule mwanamke alikuwa amekwisha waficha watu hao wawili. Basi, akawaambia wajumbe hao, “Ni kweli kwamba hao watu walikuja kwangu, lakini mimi sikujua wametoka wapi. 5Wakati wa kufunga lango la mji, giza lilipoingia, hao watu waliondoka. Kule walikokwenda mimi sijui; wafuateni upesi nanyi mtawapata.” 6Lakini Rahabu alikuwa amewapandisha hao wapelelezi kwenye paa na kuwaficha kwa mabua ya kitani aliyokuwa ameyatandaza huko paani. 7Basi, wale watu waliotumwa na mfalme wakawafuatia kwa kupitia njia iliyokuwa imeelekea kwenye vivuko vya Yordani. Na mara tu walipoondoka mjini, lango la mji likafungwa. 8Rahabu akawaendea hao wapelelezi juu darini kabla hawajalala, 9akawaambia, “Mimi ninajua kwamba Mwenyezi-Mungu amewapa nchi hii; tumekumbwa na hofu juu yenu na wakazi wote wa nchi hii wamekufa moyo kwa sababu yenu. 10Taz Kut 14:21; Hes 21:21-35 Maana tumesikia jinsi Mwenyezi-Mungu alivyoyakausha maji ya bahari ya Shamu mbele yenu mlipotoka nchi ya Misri, na jinsi mlivyowatendea wafalme wawili wa Waamori waliokuwa ngambo ya mto Yordani, yaani Sihoni na Ogu, ambao mliwaangamiza kabisa. 11Mara tu tuliposikia mambo hayo, tulikufa moyo kabisa kwa sababu yenu, tukaishiwa nguvu kabisa. Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, ndiye Mungu juu mbinguni na chini duniani! 12Kwa hiyo basi, tafadhali mniapie kwa jina la Mwenyezi-Mungu kwamba mtanitendea kwa wema mimi na jamaa yangu kama vile mimi nilivyowatendeeni kwa wema, na mnipe uthibitisho kamili. 13Ahidini kwamba mtamsalimisha baba yangu na mama yangu, kaka zangu na dada zangu, na jamaa yao yote; hamtakubali tuuawe!”
14Wale watu wakamjibu, “Uhai wenu ni uhai wetu! Kama hamtaifichua siri yetu, Mwenyezi-Mungu atakapotupa nchi hii, tutakutendea kwa wema na uaminifu.”
15Basi, Rahabu akawashusha hao watu kwa kamba kupitia dirishani, kwa kuwa nyumba yake ilikuwa imejengwa ikiambatana na ukuta wa mji wa Yeriko. 16Akawaambia: “Nendeni mlimani mkajifiche huko ili wanaowafuatia wasiwakute. Kaeni huko kwa muda wa siku tatu, mpaka wanaowafuatia watakapokuwa wamerudi mjini, kisha mwende zenu.” 17Hao watu wakamwambia, “Sisi tutalitimiza kabisa jambo ulilotufanya tuahidi kwa kiapo. 18Tutakapokuja katika nchi hii, funga kamba hii nyekundu kwenye dirisha ambalo umetuteremshia. Uwakusanye hapa kwako baba yako, mama yako na kaka zako na jamaa yote ya baba yako. 19Lakini mtu yeyote akitoka nje ya nyumba yako na kwenda mitaani hatutakuwa na lawama juu ya kifo chake. Lakini kama mtu yeyote atakayekuwamo ndani ya nyumba yako akiguswa tu, basi lawama ya kifo chake itakuwa juu yetu. 20Lakini kama ukimwambia mtu yeyote juu ya shughuli hii yetu, basi, sisi hatutabanwa na kiapo ulichotufanya tukuapie.” 21Naye akawaambia “Na iwe jinsi mlivyosema.” Kisha akawaruhusu waende zao, nao wakaondoka. Naye akaifunga ile kamba nyekundu dirishani.
22Wapelelezi hao waliondoka wakaenda milimani. Walikaa huko kwa muda wa siku tatu mpaka wale waliokuwa wanawafuatia waliporudi mjini Yeriko, baada ya kuwatafuta na kukosa kuwaona. 23Basi, hao wapelelezi wawili wakashuka kutoka milimani, wakavuka mto na kumwendea Yoshua, mwana wa Nuni; wakamwambia yote yaliyowapata. 24Wakamwambia “Hakika Mwenyezi-Mungu ameitia nchi yote mikononi mwetu. Tena wakazi wa nchi hiyo wamekufa moyo kwa sababu yetu.”


Yoshua 2;1-24

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Tuesday 10 October 2017

Kikombe Cha Asubuhi ;Leo tunaanza Kitabu cha Yoshua 1..




Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Haleluyah..!Tunamshukuru Mungu kwa kumemaliza kitabu
cha 

Kumbukumbu la Sheria  (Kumbukumbu la Torati katika tafsiri nyingine)

Ni matumaini yangu tumekuwa pamoja katika kujifunza mengi
katika kitabu kilichopita na vinginevyo huko nyuma..
Mungu wetu yu mwema sana,Si kwa nguvu zetu wala si kwa uwezo
wetu ni kwa Neema yake Mungu katuwezesha kuwa na utaratibu huu.
Basi kufikia mwisho na isiwe mwisho wa kusoma tena..
Hapana tujiwekee  muda wa kusoma na kurudia pia huko tulikopita
ili tuweze kuhifadhi ,kujikumbusha na kujifunza zaidi..
Tuzidi kumuomba Mungu wetu akatupe Neema,Kiu,Shauku
zaidi ya kusoma Neno lake na kusimamia Amri na Sheria zake..
Neno la uhai

Habari hii yahusu Neno la uhai lililokuwako tangu mwanzo. Sisi tumepata kulisikia na kuliona kwa macho yetu wenyewe; tulilitazama na kulishika kwa mikono yetu wenyewe. Uhai huo ulipotokea sisi tuliuona na sasa tunasema habari zake na kuwaambieni juu ya uhai huo wa milele uliokuwa kwa Baba na uliodhihirishwa kwetu. Tulichokiona na kukisikia ndicho tunachowatangazieni nyinyi pia, ili nanyi mpate kushirikiana nasi katika umoja tulio nao na Baba na Mwanae Yesu Kristo. Tunawaandikia nyinyi mambo haya kusudi furaha yetu ikamilike.
Baba wa Mbinguni akatupe maalifa,uelewa tunapoenda kuanza kusoma
 kitabu cha "YOSHUA",Mungu wetu akawe nasi katika kitabu hiki
na vingine vijavyo..


Mungu ni mwanga

Basi, habari tuliyoisikia kwake Yesu na tunayowahubirieni ndiyo hii: Mungu ni mwanga na hamna giza lolote ndani yake. Tukisema kwamba tuna umoja naye, na papo hapo tunaishi gizani, tutakuwa tumesema uongo wala hatuishi kwa ukweli kwa maneno na matendo. Lakini tukiishi katika mwanga, kama naye alivyo katika mwanga, basi, tutakuwa na umoja sisi kwa sisi, na damu yake Yesu Kristo, Mwanae, inatutakasa dhambi zote. Tukisema kwamba hatuna dhambi, tunajidanganya wenyewe, na ukweli haumo ndani yetu. Lakini tukiziungama dhambi zetu, basi, Mungu ni mwaminifu na mwadilifu, naye atatusamehe dhambi zetu na kututakasa uovu wote. Tukisema kwamba hatujatenda dhambi, tutakuwa tumemfanya Mungu mwongo, na neno lake halimo ndani yetu.

Tumshukuru Mungu wetu kwa wema na fadhili zake kwetu..
Tumshukuru Mungu kwa ulinzi wake kwetu wakati wote..
Asante Baba wa Mbinguni kwa mema meengi
 uliyotutendea na unayoendelea kututendea...

Utukuzwe Mungu wetu,Usifiwe Baba wa Mbinguni,Uhimidiwe Jehovah..
Unastahili kuabudiwa Yahweh,Unasthahili Mungu wetu..
Hakuna kama wewe Baba wa Mbinguni,Baba wa Baraka,Baba wa Upendo
Baba wa Faraja,Mfariji wetu,Mungu mwenye huruma..
Unatosha Yahweh,Matendo yako ni makuu sana,Matendo yako ni ya Ajabu..
Sifa na Utukufu ni wako Mungu wetu..



Mungu wetu tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha
na kujiachilia mikononi mwako Baba wa Mbinguni..
Tunaomba utusamehe makosa yetu yote tuliyoyafanya
 kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza
kuwasamehe wale wote waliotukosea..
Yahweh tunaomba utuepushe katika majaribu Mungu wetu
 utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote..
Baba wa Mbinguni tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu
Jehovah utufunike kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo wa
Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona..


Watoto wangu, ninawaandikieni mambo haya, kusudi msitende dhambi. Lakini, ikijatokea mtu akatenda dhambi, tunaye mmoja ambaye hutuombea kwa Baba, ndiye Yesu Kristo aliye mwadilifu kabisa. Kristo ndiye sadaka iondoayo dhambi zetu; wala si dhambi zetu sisi tu, bali pia dhambi za ulimwengu wote. Tukizitii amri za Mungu, basi, tunaweza kuwa na hakika kwamba tunamjua. Mtu akisema kwamba anamjua, lakini hazitii amri zake, basi mtu huyo ni mwongo, na ukweli haumo ndani yake. Lakini mtu yeyote anayeshika neno la Mungu, huyo ndiye aliye na upendo kamili wa Mungu ndani yake. Hivi ndivyo tunavyoweza kuwa na hakika kwamba tunaungana naye: Mtu yeyote anayesema kwamba ameungana na Mungu, anapaswa kuishi kama alivyoishi Yesu Kristo.
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Biashara,masomo na vyote tunavyoenda kufanya/kutenda
Mungu wetu tukatende kama inavyokupendeza wewe..
Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu ukatupe nasi neema ya kuweza kuwabariki
wenye kuhitaji..
Mungu wetu tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Baba wa Mbinguni ukatupe sawasawa na mapenzi yako..

Mfalme wa Amani tunaomba Amani yako ikatawale katika
Nyumba/ndoa zetu,watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote
wanaotuzunguka,Mungu wetu pendo lako likadumu,furaha ikatawale
hekima na busara ziwe nasi,utuwema na fadhili visipungue
msamaha na kusamehe tunapokosa kuelewana tukaelimishane
kwa upendo na Amani,tuchukuliane na kuhurumiana..
Mungu wetu ukatupe Neema ya kusimamia Neno lako
Amri na Sheria zako siku zote za maisha yetu..
Ukatufanye chombo chema nasi tukatumike sawasawa na
mapenzi yako..


Wapenzi wangu, amri hii ninayowaandikieni si amri mpya; ni amri ileile ya zamani mliyokuwa nayo tangu mwanzo. Amri hiyo ya zamani ni ule ujumbe mliousikia. Hata hivyo, amri hii ninayowaandikieni ni amri mpya, na ukweli wake unaonekana ndani ya Kristo na ndani yenu pia. Maana giza linatoweka, na mwanga wa kweli umekwisha anza kuangaza. Yeyote asemaye kwamba yumo katika mwanga, lakini anamchukia ndugu yake, mtu huyo bado yumo gizani. Yeyote ampendaye ndugu yake yuko katika mwanga, na hamna chochote ndani yake kiwezacho kumkwaza mtu mwingine. Lakini anayemchukia ndugu yake yumo gizani; anatembea gizani, na hajui anakokwenda, maana giza limempofusha. Ninawaandikieni nyinyi watoto kwa kuwa dhambi zenu zimeondolewa kwa jina la Kristo. Nawaandikieni nyinyi kina baba kwani mnamjua yeye ambaye amekuwako tangu mwanzo. Nawaandikieni nyinyi vijana kwa sababu mmemshinda yule Mwovu. Nawaandikieni nyinyi watoto kwa sababu mnamjua Baba. Nawaandikieni nyinyi kina baba kwa kuwa mnamjua yeye ambaye amekuwako tangu mwanzo. Nawaandikieni nyinyi vijana kwa sababu mna nguvu; neno la Mungu limo ndani yenu na mumemshinda yule Mwovu. Msiupende ulimwengu, wala chochote kilicho cha ulimwengu. Mtu anayeupenda ulimwengu, upendo wa Baba hauwezi kuwamo ndani yake. Vitu vyote vya ulimwengu – tamaa mbaya za mwili, vitu wanavyoviona watu na kuvitamani, majivuno yasababishwayo na mali – vyote hivyo havitoki kwa Baba, bali vyatoka kwa ulimwengu. Ulimwengu pamoja na vitu vyake vyote vyenye kutamanika unapita; lakini mtu atendaye atakalo Mungu, anaishi milele.

Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..

Baba wa Mbinguni tunaomba ukawaguse kwa mkono wako
wenye nguvu wote wanaopitia vikwazo,majaribu,shida/tabu
wagonjwa,wenye njaa,waliokatika vifungo mbalimbali
Mungu wetu ukawaponye kimwili na kiroho pia
wakapate tumaini jipya,amani na wakasimame tena
ukawape neema ya kuweza kujiombea,kutambua/kujitambua
na kufuata nja zako nazo ziwaweke huru..


Watoto, mwisho u karibu! Mlikwisha sikia kwamba mpinzani wa Kristo anakuja, na sasa wapinzani wengi wa Kristo wamekwisha fika, na hivyo twajua kwamba mwisho u karibu. Watu hao wametokea kati yetu lakini hawakuwa kweli wa kwetu na ndiyo maana walituacha; kama wangalikuwa wa kwetu, wangalibaki nasi. Lakini waliondoka, wakaenda zao, kusudi ionekane wazi kwamba hawakuwa kamwe wa kwetu. Nyinyi, lakini, mlipata kumiminiwa Roho Mtakatifu na Kristo, na hivyo mnaujua ukweli. Basi, nawaandikieni, si kwa kuwa hamwujui ukweli, bali kwa sababu mnaujua; na pia mnajua kwamba uongo wowote haupatikani katika ukweli. Mwongo ni nani? Ni yule anayekana kwamba Yesu ni Kristo. Mtu wa namna hiyo ni mpinzani wa Kristo – anamkana Baba na Mwana. Maana yeyote anayemkana Mwana, anamkana pia Baba; na yeyote anayemkubali Mwana, anampata Baba pia. Basi, ujumbe ule mliousikia tangu mwanzo na ukae mioyoni mwenu. Kama ujumbe huo mliousikia tangu mwanzo ukikaa ndani yenu, basi, mtaishi daima katika umoja na Mwana na Baba. Na ahadi aliyotuahidia sisi ndiyo hii: Uhai wa milele. Nimewaandikieni mambo haya kuhusu wale wanaotaka kuwapotosha nyinyi. Lakini, kwa upande wenu nyinyi, Kristo aliwatia mafuta kwa Roho wake. Na kama Roho huyo akiendelea kukaa ndani yenu, hamhitaji kufundishwa na mtu yeyote. Maana yeye anawafundisheni kila kitu, na mafundisho yake ni ya kweli, si ya uongo. Basi, shikeni mafundisho ya huyo Roho na kubaki katika muungano na Kristo. Naam, watoto, kaeni ndani yake kusudi wakati atakapotokea tuwe hodari bila kuwa na sababu ya kujificha kwa aibu siku ya kuja kwake.

Asante Mungu wetu yote tunayaweka mikononi mwako
Tukishukuru na kuamini Mungu wetu u pamoja nasi..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!
Wapendwa katika Bwana niwatakiwe Amani ya Bwana..
iwe nanyi,Baraka na upendo wa Kristo uwe nanyi
muingiapo/mtokapo Mungu awe nanyi daima..
Nawapenda.


Mungu anamwamuru Yoshua kuiteka nchi ya Kanaani

1Baada ya kifo cha Mose, mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, Mwenyezi-Mungu alimwambia Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Mose: 2“Mtumishi wangu Mose amefariki, sasa vukeni mto Yordani, wewe pamoja na Waisraeli wote hadi kwenye nchi ile ambayo ninawapa. 3Kila mahali mtakapokanyaga nimewapeni kama nilivyomwahidi Mose. 4Mipaka ya nchi yenu itakuwa hivi: Kusini ni jangwa, kaskazini ni milima ya Lebanoni, mashariki ni mto ule mkubwa Eufrate, kupitia nchi yote ya Wahiti hadi bahari ya Mediteranea upande wa magharibi. 5Hakuna mtu atakayekushinda siku zote za maisha yako. Nitakuwa pamoja nawe kama nilivyokuwa pamoja na Mose. Daima nitakuwa nawe wala sitakuacha kamwe. 6Uwe imara na hodari kwa kuwa wewe utawaongoza watu hawa kuirithi nchi ambayo niliwaahidi wazee wao kuwa nitawapa. 7Ila tu, uwe imara na hodari; uwe mwangalifu na kuzingatia sheria yote aliyokuamuru mtumishi wangu Mose. Fuata kila sehemu ya sheria hiyo nawe utafanikiwa popote uendapo. 8Hakikisha kuwa hutakisahau kamwe kitabu hiki cha sheria; bali kila siku utajifunza kitabu hiki, mchana na usiku, ili upate kutekeleza yote yaliyoandikwa humu, nawe utafanikiwa na kustawi popote uendapo. 9Kumbuka kuwa mimi nimekuamuru uwe imara na hodari. Usiogope wala usifadhaike kwa kuwa mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, niko pamoja nawe popote uendapo.”

Yoshua anawatayarisha watu kuvuka mto Yordani

10Kisha Yoshua akawaamuru viongozi wa watu, 11“Piteni katika kambi na kuwaamrisha watu watayarishe chakula, kwa kuwa baada ya siku tatu mtavuka mto Yordani, kwenda kuimiliki nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu anawapeni iwe mali yenu.”
12 Taz Hes 32:28-32; Kumb 3:18-20; Yosh 22:1-6 Yoshua akawaambia watu wa kabila la Reubeni na Gadi na nusu ya kabila la Manase: 13“Kumbukeni lile jambo ambalo Mose, mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, aliwaamuru akisema, ‘Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawapa mahali pa kupumzika, na atawapa nchi hii’. 14Wake zenu, watoto wenu na wanyama wenu wa kufugwa watabaki katika nchi hiyo ambayo Mose aliwapeni, ngambo ya mto Yordani. Lakini wanaume wote hodari wakiwa na silaha watavuka mto na kuwatangulia ndugu zenu. 15Mtawasaidia mpaka Mwenyezi-Mungu atakapowapa ndugu zenu pia mahali pa kupumzikia, kama alivyowapa nyinyi, nao pia wamiliki nchi ambayo wanapewa na Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Kisha mtarudi katika nchi ambayo ni mali yenu na kuimiliki, nchi ambayo mlipewa na Mose, mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, mashariki ya mto Yordani.”
16Wakamjibu Yoshua, “Mambo yote uliyotuamuru tutayafanya, na popote utakapotutuma tutakwenda. 17Kama vile tulivyomtii Mose katika mambo yote, ndivyo tutakavyokutii wewe; Mwenyezi-Mungu, Mungu wako na awe pamoja nawe kama alivyokuwa pamoja na Mose. 18Mtu yeyote atakayeasi amri yako au kukataa kutii maneno yako au jambo lolote unalomwamuru, atauawa. Wewe, lakini, uwe na nguvu na kuwa hodari.”

Yoshua 1;1-18

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Monday 9 October 2017

Kikombe Cha Asubuhi Kumbukumbu la Sheria 34 (Kumbukumbu la Torati katika tafsiri nyingine)




Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Haleluyah..!Haleluyah..!Haleluyah..!Mungu wetu yu mwema sana..
Tumshukuru Mungu wetu katika yote..
Mtakatifu..!Mtakatifu..!Mtakatifu..!Baba wa Mbinguni..
Mungu wetu,Muumba wetu,Muumba wa Mbingu na Nchi na vyote vinavyoonekana na visivyo onekana..
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..!
Muweza wa yote,Hakuna kama wewe,Unastahili sifa,
Unastahili kuabudiwa,Unasthahili kutukuzwa,unastahili ee Mungu..!
Uhimidiwe Jehovah,Unatosha Baba wa Mbinguni,
Matendo yako ni makuu sana,matendo yako ni
 ya ajabu,wewe ni mwanzo na wewe ni mwisho,Alfa na Omega..!


“Sikiliza!” Asema Yesu, “Naja upesi pamoja na tuzo nitakalompa kila mmoja kufuatana na matendo yake. Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa mwisho, mwanzo na mwisho.” Heri yao wale wanaoosha mavazi yao, wapate kuwa na haki ya kula tunda la mti wa uhai, na haki ya kuingia mjini kwa kupitia milango yake. Lakini mbwa, wachawi, wazinzi, wauaji, waabudu sanamu na wote wanaopenda kusema uongo, watakaa nje ya mji. “Mimi, Yesu, nimemtuma malaika wangu awathibitishieni mambo haya katika makanisa. Mimi ni mzawa wa ukoo wa Daudi. Mimi ni nyota angavu ya asubuhi!” Roho na Bibi arusi waseme, “Njoo!” Kila mtu asikiaye hili, na aseme, “Njoo!” Aliye na kiu na aje; anayependa, na achukue maji ya uhai bila malipo.

Asante Baba wa Mbinguni kwa wema na fadhili zako kwetu..
Asante kwa ulinzi wako kwetu  wakati wote..
Asante kwa kutuchagua na kutupa kibali cha kuendelea
kuiona leo hii Mungu wetu..
Asante kwa pumzi/uzima na ukatufanye tayari kwa majukumu yetu na kujiandaa kwa yajayo..


“Lakini, juu ya siku au saa hiyo, hakuna mtu ajuaye itakuja lini; wala malaika wa mbinguni, wala Mwana; Baba peke yake ndiye ajuaye. Kwa maana kama ilivyokuwa nyakati za Noa, ndivyo itakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Mtu. Maana nyakati hizo, kabla ya gharika kuu, watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, mpaka Noa alipoingia ndani ya ile safina. Hawakujua kuna nini mpaka ile gharika ilipotokea, ikawakumba wote. Ndivyo itakavyokuwa wakati Mwana wa Mtu atakapokuja. Wakati huo watu wawili watakuwa shambani; mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa. Kina mama wawili watakuwa wanasaga nafaka, mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa. Basi, kesheni, kwa maana hamjui siku atakayokuja Bwana wenu. Lakini kumbukeni jambo hili: Kama mwenye nyumba angejua siku mwizi atakapofika, angekesha, wala hangeiacha nyumba yake ivunjwe. Kwa hiyo, nanyi pia muwe tayari, kwa maana Mwana wa Mtu atakuja saa msiyoitazamia.”

Si kwamba sisi ni wema sana,si kwa nguvu zetu wala utashi wetu
sisi kuwa hivi tulivyo leo hii Yahweh ni kwa mapenzi yako
ni kwa neema/rehema zako Mungu wetu sisi kuwa hivi tulivyo
Sifa na Utukufu tunakurudishia wewe Mungu wetu..

Yahweh tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza, tukijishusha na tukijiachilia mikononi mwako Mungu wetu..
Tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya..
Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea..
Mungu wetu tunaomba utuepushe katika majaribu Baba 
utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote..
Yahweh tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu 
Baba utufunike kwa Damu ya mwanao mpendwa Bwana
na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti...
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona..


“Kweli nawaambieni, yeyote yule asiyeingia katika zizi la kondoo kwa kupitia mlangoni, bali hupenya na kuingia kwa njia nyingine, huyo ni mwizi na mnyanganyi. Lakini anayeingia kwa kupitia mlangoni, huyo ndiye mchungaji wa kondoo. Mngojamlango wa zizi humfungulia, na kondoo husikia sauti yake; naye huwaita kondoo wake kila mmoja kwa jina lake, na kuwaongoza nje. Akisha watoa nje huwatangulia mbele, nao kondoo humfuata, kwani wanaijua sauti yake. Kondoo hao hawawezi kumfuata mgeni, bali watamkimbia kwa sababu hawaijui sauti yake.” Yesu aliwaambia mfano huo, lakini wao hawakuelewa alichotaka kuwaambia.


Jehovah tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu,Biashara,Masomo na vyote tunavyenda kugusa kutumia Mungu wetu tunaomba ukavitakase na kuvifunika kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo..
Mungu wetu vyote tunavyoenda kufanya/kutenda   tukatende kama inavyokupendeza wewe..

Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo 
Mungu wetu nasi tunaomba utupe neema ya kuweza 
kuwabariki wenye kuhitaji,Mungu wetu tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbingu tunaomba utupe sawasawana mapenzi yako..

Mfalme wa Amani tunaomba Amani na Upendo vikatawale katika Nyumba/ndoa zetu,watoto,wazazi wetu,famila/ndugu na wote wanaotuzunguka,Mungu wetu tunaomba ulinzi wako wakati wote
Baba wa Mbimnguni tunaomba utamalaki na kutuatamia..
Yahweh tunaomba uwe nasi katika yote,Mungu wetu tunaomba mkono wako wenye nguvu ukatuguse ,ukatutakase na kutufunika kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo,Mungu wetu ukatupe neema ya kuweza kusimamia Neno lako Amri na Sheria zako siku zote za maisha yetu ,Ukatufanye chombo chema Baba nasi
tukatumike kama inavyokupendeza wewe...
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe
na kiasi..


Basi, akasema tena, “Kweli nawaambieni, mimi ni mlango wa kondoo. Wale wengine wote waliokuja kabla yangu ni wezi na wanyanganyi, nao kondoo hawakuwasikiliza. Mimi ni mlango. Anayeingia kwa kupitia kwangu ataokolewa; ataingia na kutoka, na kupata malisho. Mwizi huja kwa shabaha ya kuiba, kuua na kuharibu. Mimi nimekuja mpate kuwa na uhai – uhai kamili. “Mimi ni mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo wake. Mtu wa kuajiriwa ambaye si mchungaji, na wala kondoo si mali yake, anapoona mbwamwitu anakuja, huwaacha kondoo na kukimbia, kisha mbwamwitu huwakamata na kuwatawanya. Yeye hajali kitu juu ya kondoo kwa sababu yeye ni mtu wa mshahara tu. Mimi ni mchungaji mwema. Nawajua walio wangu, nao walio wangu wananijua mimi, kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo Baba. Mimi nayatoa maisha yangu kwa ajili yao.
Baba wa Mbinguni tazama wenye shida/tabu,wagonjwa,wenye njaa waliokata tamaa,waliokatawaliwa,walioumizwa,walio katika
vifungo vya yule mwovu,wote wataabikao,
wanaopitia magumu/majaribu mbali mbali,Mungu wetu tunaomba ukawaguse na mkono wako wenye nguvu,Baba ukawape uponyajiwa mwili na roho pia, Mungu wetu ukawasimamishe wote walioanguka,
 Mungu wetu ukasikie kulia kwao Baba ukawafute
machozi ya watoto wako,Mungu wetu ukawape neema ya kuweza kujiombea na kufuata njia zako nazo ziwaweke huru..
Baba wa Mbinguni ukawape msamaha wale wote waliokwenda kinyume nawe,Mungu wetu wakuombapo kwa imani Baba ukawape Amani na kupokea sala/maombi yao..




Tena ninao kondoo wengine ambao hawamo zizini humu. Inanibidi kuwaleta hao pia, nao wataisikia sauti yangu, na kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja. “Baba ananipenda kwani nautoa uhai wangu ili nipate kuupokea tena. Hakuna mtu anayeninyanganya uhai wangu; mimi nautoa kwa hiari yangu mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa na uwezo wa kuuchukua tena. Hivi ndivyo Baba alivyoniamuru nifanye.” Kukawa tena na mafarakano kati ya Wayahudi kwa sababu ya maneno haya. Wengi wao wakasema, “Ana pepo; tena ni mwendawazimu! Ya nini kumsikiliza?” Wengine wakasema, “Haya si maneno ya mwenye pepo. Je, pepo anaweza kuyafumbua macho ya vipofu?”

Asante Mungu wetu yote tunayaweka mikononi mwako..
Tukiamini na kushukuru daima..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!!

Asanteni sana wapendwa katika Bwana..
Mungu wetu aendelee kuonekana kwa kila jambo
mfanyalo,naye akawape Baraka na kuwaongezea zaidi
ya mnapojitoa,msipungukiwe katika mahitaji yenu 
Baba wa Mbinguni  akawape kama inavyompendeza yeye..

Nawapenda.


Kifo cha Mose

1Basi, Mose akaondoka kwenye tambarare ya Moabu, akaenda mlimani Nebo, akapanda kilele cha Pisga kilicho mkabala wa Yeriko. Hapo Mwenyezi-Mungu akamwonesha nchi yote: Toka Gileadi mpaka Dani; 2eneo lote la Naftali, eneo la Efraimu na Manase, eneo lote la Yuda mpaka Bahari ya Mediteranea; 3nyika ya Negebu na eneo la nyika ya bonde la Yeriko, mji wa mitende, mpaka Soari. 4Kisha Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Hii ndiyo nchi ile niliyomwapia Abrahamu, Isaka na Yakobo kwamba nitawapa wazawa wao. Nimekuonesha uione kwa macho yako mwenyewe, lakini hutafika huko.”
5Basi, Mose mtumishi wa Mwenyezi-Mungu akafariki huko nchini Moabu, kama Mwenyezi-Mungu alivyokuwa amemesema. 6Mwenyezi-Mungu akamzika34:6 akamzika: Kufuatana na baadhi ya hati za Kigiriki; Kiebrania: Akazika. katika bonde la Moabu, mkabala na mji wa Beth-peori; lakini mpaka leo, hakuna mtu ajuaye mahali alipozikwa. 7Mose alikuwa na umri wa miaka 120 alipofariki; macho yake yalikuwa hayajafifia, na alikuwa timamu na mwenye nguvu. 8Waisraeli waliomboleza kifo chake kwa muda wa siku thelathini kwenye nchi tambarare ya Moabu. Kisha siku za matanga na maombolezo ya kifo chake zikaisha.
9Yoshua mwana wa Nuni alijaa roho ya hekima, kwa kuwa Mose alikuwa amemwekea mikono yake. Hivyo Waisraeli walimtii Yoshua na kufuata amri ambazo Mwenyezi-Mungu alimpa Mose.
10Hapajatokea tena nabii katika Israeli kama Mose, ambaye Mwenyezi-Mungu aliongea naye ana kwa ana. 11Hakuna nabii mwingine ambaye alifanya ishara na miujiza kama ile ambayo Mwenyezi-Mungu aliyomtuma Mose afanye juu ya mfalme wa Misri, wakuu wake na nchi yake yote. 12Hakuna nabii mwingine ambaye amefanya mambo makuu na ya kutisha kama alivyofanya Mose mbele ya Waisraeli wote.



Kumbukumbu la Sheria 34:1-12


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.