Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday 27 March 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mwanzo48...

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?
Tumshukuru Mungu kwa mema mengi aliyotutendea/anayoendelea kututenda..

Heri wote wamchao Mwenyezi-Mungu, wanaoishi kufuatana na amri zake. Utapata matunda ya jasho lako, utafurahi na kupata fanaka. Mkeo atakuwa kama mzabibu wa matunda mengi nyumbani mwako; watoto wako kama chipukizi za mzeituni kuzunguka meza yako. Naam, ndivyo atakavyobarikiwa mtu amchaye Mwenyezi-Mungu. Mwenyezi-Mungu akubariki kutoka Siyoni! Uione fanaka ya Yerusalemu, siku zote za maisha yako. Uishi na hata uwaone wajukuu zako! Amani iwe na Israeli!
Mtakatifu Mtakatifu Mtakati.. Baba Wa Mbinguni,Muumba wetu,Mungu wetu,Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..!!! Wewe ni Mwanzo wewe ni Mwisho Hakuna wa kufanana nawe..
Asante kwa kutuchagua  na kutupa tena Kibali cha kuiona Leo hii Baba wa Mbinguni..Tunaanza siku/wiki hii nawe Mungu wetu, Ukaibariki katika Kazi zetu,Biashara,Masomo, Vilaji/Vinywaji,Tuingiapo/Tutokapo, Hatua zetu ziwe nawe Mfalme wa Amani..
Roho Mtakatifu akatuongoze kwenye kunena/kutenda..Ukatufanye chombo chombo chema na ukatutumie sawasawa na Mapenzi yako Yahweh..!!

Usiache Mguu wetu ukasogezwa Baba wa Mbingu, Utupe Afya njema,Akili ya kujitambua/kutambua Baba..Ukabariki ridhiki zetu Baba ziingiapo/zitokapo Mfalme wa Amani..
Utusamehe pale tulipokwenda kinyume nawe Mfalme wa Amani
Nasi tupe Neema ya kuweza kusameheana Baba..
Baba wa Mbinguni Ukawaguse/Kuwaponya wote wanaopitia Magumu/Majaribu,Vifungo vyovyote vya mwovu na uonevu Baba,Wagonjwa,Wenye Shida/Tabu, Wafiwa wakawe mfariji wao Baba..
Tunajinyenyekeza na kujiachilia mikononi mwako Jehovah..!
Sifa na utukufu ni wako, wema na fadhili ni zako..
Upendo na Furaha vipo kwako..Uponyaji na Amani vipo nawe Yahweh..!!

Tunashukuru na Kuamini wewe ni Bwana na Mwokozi wetu..
Amina...!!
Mungu awabariki Sana.




Yakobo anawabariki Efraimu na Manase

1Baada ya hayo, Yosefu alipewa habari kwamba baba yake ni mgonjwa. Hivyo, akawachukua wanawe wawili, Manase na Efraimu, akaenda nao kwa baba yake. 2Yakobo alipofahamishwa kwamba mwanawe Yosefu amefika kumwona, akajitahidi kuinuka, akaketi kitandani. 3Yakobo akamwambia Yosefu, “Mungu mwenye nguvu alinitokea nilipokuwa kule Luzu katika nchi ya Kanaani, akanibariki. 4Aliniambia, ‘Tazama, nitakufanya uwe na wazawa na uongezeke; nitakufanya uwe babu wa jamii kubwa za watu. Ardhi hii nitawapa wazawa wako, waimiliki milele.’” 5Yakobo akaendelea kusema, “Wanao wawili uliowapata hapa Misri kabla sijafika, ni wanangu; Efraimu na Manase watakuwa wangu kama walivyo Reubeni na Simeoni. 6Lakini, watoto utakaopata baadaye watakuwa wako; kwa jina la ndugu zao wataitwa katika urithi wao. 7Taz Mwa 35:16-19 Naamua hivyo kwa sababu ya mama yako, Raheli. Nilipokuwa narudi kutoka Padani yeye alifariki katika nchi ya Kanaani, tukiwa karibu kufika Efratha, akaniachia huzuni. Basi, nikamzika papo hapo, kando ya njia iendayo Efratha, yaani Bethlehemu.”
8Israeli alipowaona wana wa Yosefu, akamwuliza, “Ni akina nani hawa?” 9Yosefu akamjibu baba yake, “Hawa ni wanangu alionijalia Mungu nikiwa huku.” Israeli akasema, “Tafadhali, walete karibu nipate kuwabariki.” 10Macho ya Israeli yalikuwa hayaoni vizuri kwa sababu ya uzee. Basi, Yosefu akawasogeza wanawe karibu na baba yake, naye akawabusu na kuwakumbatia. 11Kisha Israeli akamwambia Yosefu, “Sikutazamia kuuona uso wako tena; lakini, kumbe, Mungu amenijalia hata kuwaona watoto wako!” 12Hapo Yosefu akawaondoa wanawe kwenye magoti ya baba yake, kisha akainama kwa heshima. 13Yosefu akawainua wanawe wawili, Efraimu katika mkono wake wa kulia, akimwelekeza kwenye mkono wa kushoto wa baba yake, na Manase katika mkono wake wa kushoto, akimwelekeza kwenye mkono wa kulia wa baba yake, akawasogeza kwa babu yao. 14Lakini Israeli akaipishanisha mikono yake: Mkono wake wa kulia akauweka juu ya kichwa cha Efraimu, ingawa alikuwa mdogo, na mkono wake wa kushoto akauweka juu ya kichwa cha Manase, aliyekuwa mzaliwa wa kwanza. 15Kisha Israeli akambariki Yosefu, akisema,
“Mungu ambaye babu zangu
Abrahamu na Isaka walimtii maishani mwao,
Mungu ambaye ameniongoza maishani mwangu hadi leo,
16na malaika ambaye aliniokoa katika mabaya yote,
na awabariki vijana hawa!
Jina langu na majina ya wazee wangu, Abrahamu na Isaka,
yadumishwe katika vijana hawa;
nao waongezeke kwa wingi duniani.”
17Yosefu alipoona kwamba baba yake ameuweka mkono wake wa kulia juu ya kichwa cha Efraimu hakupendezwa. Basi, akaushika mkono wa baba yake, akitaka kuuondoa juu ya kichwa cha Efraimu auweke juu ya kichwa cha Manase. 18Akamwambia baba yake, “Sivyo, baba! Huyu hapa ndiye mzaliwa wa kwanza. Tafadhali, uweke mkono wako wa kulia juu ya kichwa chake.” 19Lakini baba yake akakataa, akisema, “Najua, mwanangu, najua. Wana wa Manase pia watakuwa taifa kubwa na mashuhuri. Hata hivyo, ndugu yake mdogo atakuwa mkuu kuliko yeye, na wazawa wake watakuwa mataifa mengi.” 20Taz Ebr 11:21 Basi, Israeli akawabariki siku hiyo, akisema,
“Waisraeli watayatumia majina yenu kubarikia,
watasema, ‘Mungu akutendee mema kama Efraimu na Manase!’”
Ndivyo Israeli alivyomweka Efraimu mbele ya Manase.
21Kisha Israeli akamwambia Yosefu, “Kama uonavyo, mimi niko karibu kufa. Hata hivyo, Mungu atakuwa pamoja nanyi, na kuwarudisheni katika nchi ya babu zenu. 22Zaidi ya hayo, nimekupa wewe, wala si ndugu zako, eneo moja milimani,48:22 eneo moja milimani: Kiebrania: Shekemu. nililowanyanganya Waamori kwa upanga na upinde wangu.”
Mwanzo48;1-22

Bible Society of Tanzania

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: